NINAFURAHI na kushukuru kwa kupata fursa hii ya kutoa salamu na pongezi zangu za dhati kwa Rais mstaafu Daniel Toroitich arap Moi wakati akitimiza umri wa miaka 90. Hakika Moi ni nembo, mtu mashuhuri na kizazi adimu cha viongozi wa Afrika.Kwa karibu miaka minane, tulifanya kazi kwa karibu na kwa amani kama viongozi wa nchi zetu; Kenya na Tanzania, na katika muktadha wa Ukanda wa Maziwa Makuu, kukuza ... Habari Kamili
JK Aitaka Afrika Kuungana Kukabiliana na Tabia Nchi
RAIS Jakaya Kikwete, amesema nchi za Afrika hazina budi kuungana na kuchukua hatua za kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa pamoja.Hayo aliyasema juzi mjini Malabo, nchini hapa alipokuwa anafungua mkutano wa wakuu wa nchi 11 zinazounda Kamati ya Mazingira ya nchi za Umoja wa Afrika (CAHOSCC).“Suala la Tabia Nchi barani Afrika ni changamoto na fursa pia kwani kama tukifanya uamuzi ... Habari Kamili
JWTZ Kulinda Amani Mataifa ya Nje
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa kutoa ushirikiano wa ulinzi na amani katika mataifa yenye matatizo ya amani.Hayo aliyasema jijini Dar es Salaam jana, wakati akizindua Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi na Amani, kilichojengwa kwa msaada wa Serikali ya Canada na kulenga kutoa mafunzo maalumu kwa maofisa wa Jeshi wa ... Habari Kamili